Quantcast
Channel: Best Hope Media™
Viewing all 734 articles
Browse latest View live

JE, UNAWAKUMBUKA HAWA JAMAA, NI MA SUPER NYOTA MKOA WA MOROGORO FIESTA 2013

$
0
0

Kulia (anayeongea kwenye simu) ni Rama wa Kitaa na kushoto mwenye tabasamu kali ni Hamis K, msanii mwenye ngoma kazaa kali zinazobamba kwenye radio stations na television mbalimbali. Ukizungumzia ngoma ya Kombolela basi utakuwa hujamsahau Hamis K.


KUMBE LADY JAYDEE NAYE YUMO KWENYE KARATE, HEBU CHEKI ANAVYO ZIPIGA HAPA KWENYE MAZOEZI

$
0
0
PICHA ZOTE ZINAONYESA BAADHI YA STYLE MBALIMBALI ANAZOJIFUNZA KATIKA MAFUNZO HAYO. NI NIA NZURI NA INABIDI LIWE NI SOMO ZURI KWA WASANII WENGINE ILI IWEZE KUWASAIDIA KUIMARISHA AFYA ZAO NA HATA KUWA WEPESI MAJUKWAANI NA SEHEMU NYINGINE MBALIMBALI ZA KAZI.

CHELSEA YAIVURUGA LIVERPOOL MABAO 2 KWA NUNGE NA KUWAFANYA KUWA WAPILI KUTOKA KILELENI KATIKA LIGI YA UINGEREZA KWA POINTI 78

$
0
0

Baada ya kujishindia mechi hiyo kwa kishindo, Chelsea wako wapili kutoka kileleni kwa kujikusanyia pointi 78 ikitanguliwa na Liverpool ikiwa na pointi 80 na kuwafanya kuwa vinara katika ligi hiyo. Mabao ya Chelsea yametiwa nyavuni na mshambuliaji machachari kabisa Demba Ba and Willian. Manchester City ipo katika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 74, huku Arsenal wakiendelea kuwa katika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 70 kibindoni. Everton katika nafasi ya 5 wakiwa na pointi 69 mkononi.

MSANII KUTOKA KENYA KEKO MBIONI KUACHIA VIDEO MPYA, HICHI NDICHO ALICHOKIPOST MTANDAONI

$
0
0
Keko kwa sasa yupo chini la lebo kubwa duniani ya Sonny Music inayowasimamia wasanii kukota pande zote za dunia.
Hichi ndicho alichopost kupitia akaunti yake ya facebook ya kekomusic kuhusiana na video yake mpya.
"Just seen the new Keko Video_Till eye say Cut, are You ready though?"


NANI KAMFUNIKA MWENZAKE KATI YA RIHANNA NA NICK MINAJ, HII ILIKUWA KWENYE TUZO ZA MTV

$
0
0
n1

n2 n3
n4
 n6
NANI KAKUKOSHA HAPO KATI YA RIRI NA NICK?

HIVI NDIVO MECHI YA VALENCIA NA ATLETICO MADRID ILIVOISHA KWA VALENCIA KUFUNGWA BAO 1 BILA.

$
0
0
MECHI HIYO NI YA LIGI YA UHISPANIA

POLISI ALIYEVAA NGUO ZA KUBANA HUKO KIAMBU NCHINI KENYA LINDA OKELLO AANDAMWA NA KUNAUWEZEKANO AKAFUKUZWA KAZI

$
0
0
Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii picha za askari polisi Linda Okello kutoka Kiambu huko Kenya zikilichora umbo lakena nguo ya ndani kwa uzuri zaidi kutokana na kumbana inasemekana kwa sasa polisi huyo yupo kwenye balaa kubwa la kuweza kumfukuzisha kazi. Habari hiyo ikiwa imeripotiwa na mtandao mmoja kutoka Nairobi, NairobiEposed ikisomeka "Kiambu female police officer with a tight up skirt. This is some very sexy police uniform but it might get the beautiful officer fired.. Her name is Linda Okello"
Waweza ona jinsi askari huyo alivoponzwa na umbo lake akiwa kazini.
Kiambu female police officer with a tight up skirt
Kiambu female police officer with a tight up skirt. This is some very sexy police uniform but it might get the beautiful officer fired


Pia chanzo hicho kiliandika"Now, your favorite female cop, whose name is Linda Okello, is in trouble. Apparently, its not allowed for cops to look sexy and at the same time keep law and order. She has been ordered to show why she should not be disciplined."
Pia tangu siku ya jumatatu inasemekana kumekuwa na vikao kuhusiana na suala hilo lililoonyesha kuwakera mabosi wa Linda, uliripoti mtandao huo, kama inavoonekana hapa, "Some reliable sources have said that All Police commanders were on Lind Okello’s case all Monday morning. She has moved through all chain and even seen her boss ,Grace Khaindi, call Nairobi County Commander 5 times within 1 hour wanting action taken on the bootylicious police lady."
Na baadae kunachanzo kiliripoti kuwa bosi wa Linda ameonyesha dalili za kumhamisha Linda kwenda kituo kingine cha Mandera kutoka Kiambu kama adhabu ya utovu wa nidhamu kwa kutovaa ipasavyo na maadili ya kazi.
Kwa undani zaidi, Linda Okello anaelimu ya Diploma in Criminology and Social Order (UON) na kwa sana anasoma Bachelor of Arts degree in Sociology and Peace Studies.
Pia Linda Okello yupo kazini kwa miaka 10, huku kwa sasa akiwa katika kitengo cha askari wa barabarani maarufu kama traffic huko Kiambu.

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

$
0
0
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatangaza nafazi za Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Cheti kwa Mwaka wa Masomo 2014/2015.
Kuzidownload bofya link hizo hapo chini, ya kwanza ngazi ya cheti (Certificate Grade A) na ya pili ni stashahada (Diploma).




TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.

VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.

1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
  1. Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
  2. Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
  3. Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

2: MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
  1. Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
  2. Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo kabilishi wataendelea na mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A

3: ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha ualimu Patandi:-
Mwombaji awe:
  1. Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  2. Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).

MAELEZO MUHIMU
  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
  4. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  5. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz);
  6. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  7. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:
  • Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV;
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti (kwa waombaji walioajiriwa); na
  • Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)


TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.

Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati wa takribani walimu 26,000, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/2015, wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.

VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.
1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MASOMO YA SAYANSI, HISABATI NA UFUNDI: MUDA MIAKA 2

  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na MonduliMwombaji awe amehitimu: Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
  2. Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Klerruu. Mwombaji awe amehitimu:

a.Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au
b. Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
(iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu ‘Principal Pass’ mbili katika somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’, ‘Chemistry’ au ‘Food and Nutrition’.

2: MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na English.

3: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi Jamii.
  2. Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara.
  3. Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja

Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, Basic Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Divinity’ na ‘Islamic Knowledge’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.

4: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’, ‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘Agriculture’, ‘Food and Nutrition’, ‘English’ na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.

5. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI): MUDA MIAKA 2
  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na Monduli.Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  2. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi Jamii; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  3. Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  4. Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi. Mwombaji awe: Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

6: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 2:

Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

MAELEZO MUHIMU
  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  4. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
  5. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  6. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu;

VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:

  • Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV, VI na Ufundi;
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada (kwa waombaji walioajiriwa); na
  • Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.

Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

BREAKING NEWS: BONGO MOVIE TENA - MWONGOZAJI WA FILAMU GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KWA AJARI YA GARI MKOANI MOROGOR

$
0
0

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro.
Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha  The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.
Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.
Akiwa kazini enzi za uhai wake

Batuli: - Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director......Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu
Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. ...mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen.....R.I.P George Tyson.
Agness Masogange: R.I.P  George tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako!
Flaviana Matata : This is very sad aisee,Rest In Peace Tyson.Mungu kakupenda zaidi, - monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu
Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week... tunamzika mwenzetu mwingine... George Tyson.... Dah... Im just speechless.. RIP brother... Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee.... Pole dada akee ... Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya @thembonishow .... Pigo kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha tu jamani.
Aunty Ezekiel - Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director .....Nakosa lakusema
Mohamed Mwikongi : Hakika yametufika, A film director George Otieno Tyson naye hatunae tena duniani.
George Tyson aliwahi kuwa mume wa mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa naye mtoto mmoja.
Akiwa na Mboni Mwasimbi wa The Mboni Show
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

KAMPUNI YA TIGO WATANGAZA NAFASI ZA KAZI, ZIANGALIE HAPA

$
0
0

• Responsible for managing Marketing & Sales categories and meet local targets of cost, quality, time, guarantees and services

• Responsible of efficiently managing the day to day relationship and transactions with Suppliers within Marketing & Sales categories, ensuring compliance with contracted terms and conditions, and MIC Internal Control policies

Key Responsibilities
• Develop and execute the Category Supply Strategy to achieve best in class Supplier Base

• Coordinate and negotiate requirements with local internal customers, and support them with the commercial side of enforcing contracted terms and performance

• Develop in depth industry understanding within his/her assigned Category, specifically concerning local competitive forces, breakthrough business or technology advances, and cost structure

• Support Local HoD P&SC and Procurement Manager in the development of specific category strategies and any other duties to be assigned

• Support Global P&SC Team in the development of specific category strategies, global tenders and / or negotiations

Position Requirements
• Bachelor in Business Administration,Engineerings, Technical or Economic and/or related careers
• Graduate level required, MBA desirable

KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA LEO MEI 31,2014

$
0
0
Magazeti ya leo Soma kurasa za mbele na za nyuma upate kwa kifupi yaliyojiri leo habari kitaifa ,kimataifa, michezo,burudani na udaku .
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

na millard ayo.com

PICHA ZA AJALI YA GEORGE TYSON HUKO MOROGORO

$
0
0
"Gari alilopata nalo ajali Marehemu George Tyson saa kumi na mbili jioni May 30 2014 akitokea Dodoma - Dar es salaam. picha kutoka djchokamusic.com"

Picha hizi zilipigwa masaa manne kabla@jojityson hajapata ajali iliyo chukua maisha yake. "Marehemu Geogre Tyson pichani alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino Dodoma, kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini. Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majeraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam." Msiba upo nyumbani kwa marehemu Bahari Beach.

WALIOITWA KWENYE USAILI IDARA YA UHAMIAJI

$
0
0

KUITWA KWENYE USAILI 
KAMISHNA MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI ANAWATANGAZIA KUITWA KWENYE USAILI KWA NAFASI ZA KONSTEBO WA UHAMIAJI NA KOPLO WA UHAMIAJI, USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 09.06.2014 HADI TAREHE 26.06.2014 KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA MAASKOFU (TEC) KURASINI BARABARA YA NELSON MANDELA.

Kufungua Majina ya walioitwa(pdf) BOFYA HAPA

Download attachments: uhamiaji_majina.zip

PETER MUTHARIKA RAIS MPYA MALAWI, BAADA YA KUMBWAGA MH. JOYCE BANDA

$
0
0
Mgombea wa Chama cha upinzani nchini Malawi Peter Mutharika ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais uliozua utata.
Mutharika wa Chama cha Democratic Progressive Party amepata asilimia 36.4 ya kura, imetangaza tume ya uchaguzi nchini humo.
Rais anayeondoka madarakani Joyce Banda amedai uchaguzi huo ulivurugwa.
Tume ya uchaguzi ya Malawi (MEC) iliomba siku 30 za ziada ili kura zihesabiwe upya kabla ya kutangaza matokeo.
Hata hivyo, Mahakama Kuu ilitupilia mbali ombi hilo na kutoa amri ya matokeo kutangaza siku ya Ijumaa.
"Sheria iko wazi, hakuna kuongeza muda," amesema Jaji Kenyatta Nyirenda.
Bwana Mutharika ni ndugu yake Rais Bingu wa Mutharika aliyefariki dunia mwaka 2012. Peter Mutharika alikuwa Waziri wa mambo ya nje wakati ndugu yake akiwa rais.

HICHI NDICHO ALICHOKIANDIKA MONALISA KUHUSIANA NA MSIBA WA GEORGE TYSON

$
0
0
RIP George Tyson, pole kwa Monalisa, mwanao, familia na marafiki pia.Alikua kati ya madirector bora bongo movie.Nakumbuka alikua akipenda matani sana.Mungu ampumzishe kwa amani.


ZITO KABWE AELEZA KWA KIFUPI HISTORIA YA MAMA YAKE WAKATI WA KUAAGA TAYARI KWA SAFARI YA KIGOMA

$
0
0
Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.

Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu.


nyumba ya mapumziko ya milele.
============================== ============================== =====


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza kwenye gari jeneza lenye mwili wa Saida Salum, mama mzazi wa Zitto tayari kuelekea uwanja wa ndege.



Wakazi wa jiji wakiingiza mwili wa Mama mzazi wa Zito Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Shida Salumu)katika gari tayari kwa Safari ya kuelekea Kigoma mara baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Maamul jijini Dar es Salaam jana.Marehemu anatarajiwa kuzikwa mjini kigoma

Mbunge wa Musuma Vijijini Nimrod Mkono (kulia) na Mbunge wa Bunda Stephen Wasira (kushoto) wakifariji Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zito Kabwe kwa kufiwa na Mama yake Mzazi.


Picha chini zinaonyesha baadhi ya waombolezaji waliohudhuria swala ya kuswalia Marehemu Shida Salum, Mama yake Zitto Kabwe.





Zitto kabwe akiwa na Prof Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.

Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe.

Kardinali Polycarp Pengo akiwa na Rais wa TASWA, Juma Pinto akiwa VIP JKN Airport walipokutana wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe,

Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe, Bi Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi

Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko

SIRI IMEFICHUKA, KAZI NJE NJE. SOMA HAPA UJIPATIE KAZI.

$
0
0

Kupata nafasi za ajira imekuwa ngumu siku hadi siku, hususani ukitilia maanani kuwa wahitimu wanazidi kuwa wengi na hali ngumu ya uchumi inafanya waajiri kushindwa kuongeza nafasi mpya za kazi. Hauna haja ya kukata tamaa ya kupata kazi ile unayoitarajia hata kama kuna ukiritimba mwingi katika soko la ajira kama vile watu kupeana kazi kwa kujuana, nafasi za kazi kutotangazwa  au kazi haipatikani mpaka rushwa itembee. Makala hii inaenda kujadili mambo ya msingi kwa yeyote anayetafuta kazi, uwe kwa sasa umeajiriwa unatafuta kazi mbadala au uwe hauna ajira unatafuta ajira, bila shaka mambo tunayojadili hapa yatakusaidia.
1.Mtazamo wako kuhusu ajira:
Fahamu kuwa bidhaa ni chochote kile ambacho kinatimiza mahitaji fulani. Mwenye kuhitaji bidhaa huwa tunamuita mteja.  Muajiri anatafuta mfanyakazi kwa kuwa analo hitaji la kazi fulani kukamilika, na anayo matarajio kadhaa toka kwa mfanyakazi anayemuajiri.   Hivyo wewe kama mfanyakazi mtarajiwa unayo ‘bidhaa’, yaani uwezo wako wa kutimiza majukumu fulani ambayo utatakiwa kufanya na muajiri. Kwahiyo mtazamo sahihi unaotakiwa kuwa nao wakati unatafuta kazi ni kuwa wewe ni muuzaji wa bidhaa, na muajiri wako mtarajiwa ni mteja.  Kwakuwa wapo ‘wafanyabiashara’ wengi wa hiyo bidhaa kama yako (watu wanaotafuta ajira), unahitajika basi kujipanga vema ili kumshawishi na kumfanya mteja wako  (muajiri mtarajiwa) aone kweli sababu ya kununua ‘bidhaa ‘toka kwako.
2.Wasifu wako ujitosheleze:
Ukiwa na mtazamo tuliouleza hapo juu wa kuwa wewe ni mfanyabiashara unauza bidhaa kwa mteja wako (muajiri), unatakiwa basi utumie vema wasifu wako (CV) kujieleza vema ili ‘mteja’ akukubali.Mambo ya kuzingatia katika wasifu wako ni kama yafuatavyo:-

  • Wasifu wako uendane na aina ya kazi unayo omba: Hivyo basi usiweke kila aina ya maelezo hata yale ambayo haya umuhimu na kazi husika. Mfano unaomba nafasi ya kazi ya uhasibu, lakini unaweka maelezo ya uzoefu wa sehemu tatu tofauti ya kazi za ulinzi.
  • Wasifu wako uonyeshe kweli unao uwezo wa kazi unayoiomba:  Hivyo basi usitaje tuu majina ya kampuni au asasi ulizofanya kazi na aina ya cheo ulichoshika ukiwa huko, bali eleza mambo ya msingi ambayo  ni mafanikio ya wewe kuwepo katika kampuni au asasi fulani uliyokuwepo. Mfano kwa kazi yako kama msimamizi wa ofisi, uliweza andaa mikutano  (itaje) ambayo ilikutanisha watendaji wakubwa wa kampuni yako ambapo kupitia maandalizi mazuri uliyoyafanya, kampuni yako iliweza kupendekezwa mara tatu mfulululizo kuandaa mikutano hiyo.
  • Wasifu wako uonyeshe utofauti wako wewe na watu wengine: Haitoshi kuandika katika CV yako kuwa umemaliza masomo ya ngazi ya stashahada au shahada, haitoshi kutaja kuwa umewahi kufanya kazi fulani mfano kazi ya usimamizi wa ofisi halafu ukaorodhesha majukumu ya msimamizi wa ofisi, mambo ambayo kwa ujumla yanajulikana kuwa ni majukumu ya msimamizi wa ofisi yeyote yule wa ofisi. Kumbuka wasifu wako (CV) ni nyaraka muhimu ya kumshawishi ‘mteja’ kuwa ananunua ‘bidhaa bora zaidi ya nyingine katika soko la ajira. Hivyo basi jipange kwa kuonyesha utofauti, badala ya kutaja tuu ngazi za juu za elimu ulizofanikiwa kufika, taja pia maeneo ambayo wewe kweli ‘upo mzuri’ yaani maeneo ambayo kweli haubabaishi katika ngazi hizo za elimu unazotaja. Pia kwa upande wa uzoefu wa kazi, taja mafanikio uliyokwisha pata kutoka ajira zako zilizopita, au tuseme mambo gani ‘mazito’ ulikamilisha na kusaidia ukiwa kwa waajiri wengine.

3. Fuata maelekezo kwa ufasaha:  
Unapowasilisha maombi yako ya ajira, hakikisha unafuata maelekezo yaliyotolewa katika tangazo la nafasi za kazi, kwani hata kama ni jambo dogo, utakalokosea linaweza kuchukuliwa kama sababu ya wewe kutokuwa mfanyakazi makini, hivyo kukosa hata nafasi ya kuitwa kwa usaili (interview). Mfano kama umeambiwa uorodheshe wadhamini watatu, hauna sababu ya kuorodhesha wadhamini wawili tuu. Kama umeambiwa utume maombi kwa njia ya posta, usitume maombi yako kwa barua pepe wala kupeleka kwa mkono.Hakikisha pia unafuata maelekezo ya tarehe na muda wa kuwasilisha maombi yako ya kazi. Pia zingatia maelekezo kuhusu vyeti na nyaraka nyingine unazotakiwa kuziambatanisha pamoja na barua yako ya maombi ya kazi. Kama umeambiwa utume CV yako tuu, usihangaike kutuma vitu vingine kama vyeti, na barua ya maombi ya kazi.
4.Barua ya maombi ibebe uzito:
Barua yako ya maombi ya kazi ni nafasi nyingine ya kushawishi ‘wateja’ wako kuwa kweli utawapatia huduma wanayoitaka, na kwamba watakapofanya chaguo la kukuajiri wewe watakuwa wamefanya chaguo bora kabisa. Anza kwa kueleza aina ya kazi unayoomba, umetambuaje uwepo wa nafasi hiyo ya kazi. Jieleze kwanini wewe ni chaguo lao bora kwa kulinganisha majukumu ya kazi unayoomba na ujuzi wako, uzoefu wako, na yale uliyokwisha wahi kufanikisha hapo kabla.  Kwakuwa barua ya maombi ya kazi huwa ni fupi, usiwachoshe kwa maelezo mengi, ila maelezo yako yawavutie kusoma nyaraka ulizoambatanisha kama vile CV na  vyeti .
5. Jiandae kwa ‘interview’:
Utakapopata nafasi ya kuitwa kwa usaili, usiende bila kujiandaa. Fahamu vema majukumu yanayoendana na nafasi ya kazi uliyoomba, hakikisha unakumbuka nini uliandika katika barua yako ya maombi ya kazi na CV yako. Jikumbushe mambo ya msingi kuhusu elimu ya darasani ambayo umetaja unayo. Jifunze pia maswali mbalimbali ya kisaikolojia yaulizwayo katika usaili , kama vile ‘Tuambie madhaifu yako ni yapi ?”. Unaweza jifunza jinsi ya kujibu maswali kama hayo kupitia vitabu au hata kwa ku search kwa mtandao.
6. Usisubiri nafasi za kazi zikufuate:
Amini kuwa kuna waajiri wengi ambao hawatangazi nafasi za kazi kwenye vyombo vya habari au mitandaoni. Pia wapo ambao wamekwisha tangaza lakini hawajapata watu wenye kukidhi kweli viwango vyao. Hivyo usingoje nafasi za ajira zikufuate kwa kupitia vyombo vya habari, badala yake wewe mwenyewe wasiliana na waajiri mbalimbali ukiwaeleza nia yako na uwezo wako wa kufanya kazi kwao.  Waweza tembelea ofisi za makampuni au asasi mbalimbali na pia tembelea website  na hata maonyesho ya biashara au maonyesho ya waajiri (Job Fairs). Njia nyingine ni kujenga mitandao na watu mbalimbali ambapo kupitia mitandao hiyo waweza jieleza hitaji lako la kutaka ajira. Kumbuka kama una ‘bidhaa’ bora, na ukimpata mteja mwenye kuhitaji ‘bidhaa’, bila shaka una nafasi kubwa ya kupata ajira.
7. Itunze ‘taswira’ yako:
Waajiri wengi hupenda kufahamu zaidi kuhusu mtu wanayetaka kumuajiri, sio tuu uwezo wake kiujuzi wa kazi, bali pia uaminifu wako, wewe ni mtu wa aina gani katika kujiheshimu na kujiheshimu wengine n.k. Hivyo hakikisha hauharibu ‘taswira’ yako kupitia aina ya marafiki ulionao, aina ya twitts, status, picha n.k unazoweka katika mitandao ya kijamii kama Facebook, na Twitter. Pia unapotaka kuacha kazi toka asasi fulani , jitahidi uache kwa amani, isije baadae waajiri wako wengine wakataka kujua aina gani ya mfanyakazi ulikuwa hapo kabla wakajibiwa habari isiyopendeza.

SI YA KUKOSA, CHOCHOTE ONLINE MAGAZINE SASA LIKO KWENYE MTANDAO JISOMEE HAPO.

TAASISI YA FARIDA FOUNDATION KUFANYA UZINDUZI SIKU YA TAREHE 28/06/2014

$
0
0



 Taasisi ya faridas foundation inatarajia kufanya uzinduzi wake rasmi siku ya tar 28/6/2014 siku ya jumamosi katika ukumbi wa crystal hall, blue pearl hotel, ubungo plaza kuanzia saa 6-12 jioni. Katika siku hyo taasisi itatoa misaada mbali mbali kwa walemavu ikiwemo baiskeli za walemavu, vyerehani, vifaa vya shule na vifaa vingine muhimu kwa walemavu ukiwa kama mdau au mtanzania unayeguswa na walemavu na ungependa kuhudhuria siku hyo maalumu kadi zinapatikana kwa mchango wa shilingi laki moja na kuendelea hii ikiambatana na chakula cha mchana vinywaji na burudani mbalimbali pia utakuwa umesaidia kuongeza idadi ya vifaa vitakavyotelewa kwa walemavu mbali mbali. Kutoa ni moyo sio utajiri. Endapo una kampuni au ungependa kushiriki kama kampuni au taasisi kwa kudhamini pia nafasi bado zipo wazi wasiliana nasi kupitia +255715186262 au email faridasfoundation@gmail.com

TWITTER YAMPA DIAMOND PLATNUMZ UMILIKI HALALI WA AKAUNTI YAKE @diamondplatnuz

$
0
0

Twitter umempa umiliki halali wa akaunti yake ya Twitter kwa kuwa Verified.

verifed 

Diamond Platnumz anaungana na mastar kadhaa wenye  verified kwenye akaunt zao ambao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete,Ambwene Yesaya ‘Ay’,Flavian Matata.January Makamba na baadhi ya mastaa.

katika kurasa zake za mitandao ya kijamii leo Diamond amewashukuru twitter kwa kuandika>>’Thank you Twitter', mtandao wa Twitter umempa umiliki halali wa akaunti yake ya Twitter kwa kuwa Verified.
Viewing all 734 articles
Browse latest View live




Latest Images